Breaking News

NEWS Siri Ya Samatta Kupewa Jezi Namba 77 Katika Klabu Yake Mpya Ya Genk

Mbwana Samatta
Mbwana Samatta
Baada ya mchezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu “Taifa stars” na mchezaji wa kimataifa Mbwana Ally Samatta kusaini mkataba wa miaka minne na klabu yake mpya GENK FC ya nchini Ubelgiji wa kuichezea soka klabu hiyo, alitambulishwa kwa waana habari kama ishara ya utambulisho rasmi wa Samatta klabuni hapo.
Katika utambulisho huo Samatta alikabidhiwa Jezi nambari 77, wakati katika klabu yake ya zamani ya TP Mazembe alikuwa  akitumia jezi yenye nambari 9 mgongoni, jambo ambalo Mbwana Samatta alilweza kulitolea ufafanuzi, ambapo mbwana alisema kuwa yeye anapenda kutumia jezi  nambari  7 lakini kwakuwa jezi hizo katika klabu nyingi huwa zimesha chukuliwa aliamua kuomba jezi nambari  77 kwakuwa aliamini ni mara chache watu  huchagua kuitumia nambari 77.
Samatta aliongeza kuwa hata wakati alipokuwa akiichezea TP Mazembe alikuwa akiushawishi uongozi umpatie jezi nambari 7, lakini haikuwa rahisi kwa kuwa tayari jezi namba 7 ilikuwa inamilikiwa na mtu mwingine, na hivyo katika klabu yake mpya ya GENK FC hakuona sababu ya kuomba tena jezi hiyo badala yake aliamua kuomba jezi nambari 77 kwakuwa bado ana mapenzi na namba 7.