NEWS simu Feki Zote Kufungiwa, Ingia Hapa Kuijua Ya Kwako
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa maelekezo ya kuangalia simu yako kama ni feki au origino.
Ili kujua kama simu ni origino au feki unachotakiwa ni kubonyeza *#06# ili upate namba ya IMEI, na kisha hiyo IMEI namba uitume kwenda namba 15090 ambapo utapokea ujumbe utakaokufahamisha kama simu yako ni feki au origino. Kumbuka kutuma ujumbe huo ni bure kabisa.
Mamlaka hiyo imetoa tangazo la kuwataka watumiaji wa simu kujiridhisha kama simu zao ni origino kwa kuwa inatarajia kuzifungia simu zote feki ifikapo 17.6.2016.
TCRA ndicho chombo kilichoanzishwa kisheria kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji nchini hivyo ni jukumu lako kuchukua hatua mapema kabla simu yako haijafungiwa
No comments