Breaking News

Dully Sykes: Hakuna legend ambaye hajawahi kuandikiwa nyimbo


Akiongea na Perfect katika 255 ya Clouds FM, Dully alisema kuwa wimbo wake ‘Inde’ amesaidiwa kuuandika na Raymond wa WCB. “Inde nimesaidiwa kuandika na Raymond, nyimbo nyingine ambayo nimeandikiwa ni dhahabu. Kwenye nyimbo hiyo chorus niliandika mwenyewe ila verse nilisaidiwa na msanii anaitwa Jay C ambaye alishawahi kufanya kazi na Q Chilla wimbo wa Mpiga Debe,” alisema Dully Sykes “Hakuna legend ambaye hajawahi kuandikiwa na pia huwezi kuwa Legend kama hujawahi kuandikiwa, kwasababu legend si mjivuni,” alisisitiza. Hadi sasa Inde umekuwa wimbo wenye mafanikio makubwa kwa msanii huyo.                                  

No comments