Breaking News

KUFUATIA KUKUMBWA NA TUHUMA ZA RUSHWA, RAIS JACOB ZUMA ATIMIZA AMRI ALIYOPEWA NA MAHAKAMA KUU NCHINI AFRIKA KUSINI


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, hatimae amelipa kiasi cha fedha cha takribani USD 542,000 za umma alizozitumia kufanyia ukarabati wa nyumba yake binafsi.
Mahakama Kuu nchini humo, mweiz Machi mwaka huu ilitoa msimamo kwamba Rasi Jacob Zuma alivunja katiba ya nchi na hivyo kumuamuru kulipa kiasi hicho cha fedha kilichotumika kufanyia ukarabati nyumba yake binafsi iliyoko Nkandla, Jimbo la KwaZulu Natal.
Marekebisho yaliyofanyika katika nyumba hiyo ni kwenye sehemu ya wageni, bwawa la kuogelea na mengine mengi yaliyogharimu fedha nyingi tu. Aidha, mwanzoni Zuma alisema marekebisho hayo yalifanywa kwa sababu tu za kiulinzi.
Fedha zilizolipwa na Rais ziliwekwa katika Benki ya South African Reserve Bank kama Mahakama ilivyomuamuru. Na maelezo yake ya wapi alikotoa fedha hizo yalisema amekopa. Mhazini wa benki hiyo alikubali kwa wakati wake kwamba fedha zimepokelewa.
Upinzani nchini humo wamekua wakitumia kauli mbiu ‘pay back the money’ kukumbusha wananchi kwamba ANC imetawaliwa na rushwa kubwa. Nyumba hiyo imekua nembo ya kuonyesha jinsi gani rushwa na kupendeleana katika nyazifa za juu za chama cha ANC. – DW
Picha ya nyumba ya Zuma iliyotumia fedha za Serikali kufanyiwa marekebisho:-
Image result for zuma house Nkandla, KwaZulu Natal
Image result for zuma house Nkandla, KwaZulu Natal
Image result for zuma house Nkandla, KwaZulu Natal
Image result for zuma house Nkandla, KwaZulu Natal

No comments