Breaking News

UJUMBE WA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWA WANUFAIKA MIKOPO AMBAO HAWAJAPATA KAZI AU KUAJIRIWA

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imesema kuwa haihusiki kumtafutia mnufaika wa mkopo ajira badala lake inahusika kumpatia mwanafunzi mkopo na akishamaliza muda wa masomo atatakiwa kurejesha mkopo wake.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia mtandao wa Facebook.com/eatv.tv.
“Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatoa mikopo suala la kutafuta ajira halituhusu hivyo mnufaika yoyote asiwe na kigezo kwamba hajapata kazi , hiyo siyo kazi yetu, kazi yetu ni kuwawezesha kupata elimu basi” – Mwaisobwa.
Aidha Mwaisobwa amesema pia wanufaika wote ambao walipata mikopo wanatakiwa kukatwa asilimia 8% ya pato la mwezi, na kama mtu anafanya kazi binafsi na hakatwi popote atatakiwa kutoa kiwango cha 120,000/= na kwa ambao wamenufaika na hawataki kuanza kulipa mkopo watapigwa penati ya 10% ya mkopo kwa mwaka.
Pamoja na hayo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imewataka walioomba mikopo kuvuta subira kwani Bodi inasubiri majina kutoka Tume ya Vyuo Vikuu ili Bodi ya Mikopo iweze kufahamu vyuo walivyopangiwa na kiwango cha ada ili haki iweze kutendeka kwa waombaji. – EATV

                                                          Download DJ ABASI.COM Android Application Click HERE

No comments