Breaking News

24/2/2015...MAUAJI YA KINYAMA YAIKUMBA MOROGORO, JAMAA AUA MWANAMKE WAKE GESTI

Kijana mmoja mkazi wa Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam amemua   mwanamke kikatili kwa kumnyongwa hadi kufa katika nyumba ya kulala wageni ya Stav iliyopo eneo la kichangani mjini Morogoro.

Kamanda poilsi mkoa wa Morogoro Lenard Paul amesema jeshi la polisi linamshikilia kijana atwaye Erick Bruno (30) mkazi wa Manzese baada  kumua  mwanamke aitwaye Jada Dungu mkazi wa Kichangani mjini Morogoro kwa kumnyonga hadi kufa usiku wakati wakiwa wamelala katika nyumba ya wageni na mtuhumiwa anahojiwa na atafikishwa mahakamani.
 
Nao wananchi walioshuhudia tukio hilo wamesema usiku walisikia marehemu akipiga kelele akiomba msaada ambapo walienda katika eneo la tukio katika nyumba ya kulala wageni ndipo wakavunja mlango na kufanikiwa kumkakata mtuhumiwa akijiandaa kutoroka baada ya kufanya mauaji.
 

Katika tukio jingine mtu mmoja amekutwa amekufa katika boma lisoloishi watu huku mwili wake ukiwa umeharibika katika eneo la mji mpya katika manispaa ya Morogoro ambapo kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo wamesema mtu huyo alifahamika kwa majina ya Anton Mbulu na mwili wake umechukuliwa na jeshi la polisi na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

No comments