Breaking News

27 Feb 2015 DEREVA NA UTINGO WAKE WATEKETEA KWA MOTO BAADA YA LORI LAO KUWAKA MOTO

Watu watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea   kabisa akiwemo dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar es Salaam.

Blog hii imeshuhudia kikosi cha zimamoto ambao walichukua muda   kuuzima moto huo kutokana na kusamabaa ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu kujitokezakuiba mafuta kama ilivyozoeleka.
 
Baada ya kumaliza kuuzima moto huo  hapa kikosi cha zimamoto na uokoaji wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine ili na kukata kwa kutumia mashoka mabaki ya lori hilo baada ya walioshuhudia tukio hilo kueleza kuwa watu wote waliokuwemo katika gari hawakutoka  ambapo baada ya muda miili mitatu iliokolewa ikiwa imuungua kabisa.
 
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo maderva wa malori ambapo walikua wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusufu amesema lori hilo lilikua limesheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya Petro Africa ilikua ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo ilipoteza uelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto ambapo waliofariki dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliefahamika kwa majina ya Emela na mtu mmoja ambaye bado hajaweza kufahamika mara moja.
 
Nao wananchi walishuhudia tukio hilo wameeleza jinsi tukio lilivyotokea ambapo wananchi wamelalamikia eneo hilo limekua na matukio mengi ya ajali na hivyo kuomba serikali kuona umuhimu wakuweka vituo vya zimamoto katika eneo hilo kwani magari ya zimamoto yalichukua muda mrefu kufika kwneye enelo la tukio kutokana na umbali mrefu.
 
Nae afisa mkaguzi msaidizi wa kikosi cha zimamoto Hamadi Dadi ameeleza walivyopata taraari za ajali wametumia muda mrefu kufika katika eneo la tukio ingawa wametumia muda mrefu kuzima moto huo kutokana na mafuta yaliokua yakivuja. 
 

Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na askari walionekana muda wote kwenye  eneo la tukio

No comments