Breaking News

PICHA: LORI LA MAFUTA LATEMBEA BILA YA DEREVA MJINI MOSHI

Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi wakiashangaa lori la mafuta lilotembea bila ya kuwa na dereva likitoka kituo cha mafuta cha Puma lilipokuwa limepaki kwa ajili ya kushusha mafuta.tukio hilo limetokea mchana wa leo mjini Moshi jirani na ofisi za TTCL.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa lori hilo baada ya kukata kona ya ghafla ambayo ilisaidia madhara zaidi yasitokee baada ya tanki kukata na kurudi upande wa barabarani na kisha kusimama.
Hata hivyo tukio hilo ambalo limewaduwaza watu wengi limesababisha uharibifu mdogo katika gari ndogo inayoonekana hapa.
Dereva wa lori hilo ambaye jina lake halikufahamika mara moja akijaribu kuliondoa gari hilo mara baada ya kurejea akitoka msikitini na kukuta gari liko katikati ya barabara tofauti na sehemu alikokuwa ame paki mwanzo.
Gari hilo lililokuwa na mafuta ya Petrol liliondoka katika eneo hilo bila ya tatizo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments