06 Mar 2015 Waishio Mabondeni mkoani Shinyanga watakiwa kuhama
Kutokana na Mvua zilizosababisha maafa Mkoani Shinyanga na kusababisha watu 42 Kufariki na 91 kujeruhiwa Mkuu wa mkoa huo amewataka wananchi waishio maeneo ya mabondeni kuhama ili kuepuka madhara kujitokeza kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Akitoa Tahadhari hiyo kwa wakazi wa Mkoa huo Ally Nassoro Rufunga amesema kuwa kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa walishatoa taarifa kuhusiana na mvua hizo na serikali ilichukua hatua ya kuwaelemisha wananchi waishio mabondeni kuhama na kuongeza kuwa kwa sasa wananchi wafate maagizo hayo kwa kuwa mvua zitaendelea kunyesha.
Akitoa takwimu za Ujumla za Madhara yaliyojitokeza kutokana na mvua hizo Rufunga amesema jumla ya kaya 82 zimeharibiwa na watu waliotharika ni 574 na nyumba zilizoharibika kabisa ni 137, pamoja na Mashamba na mifugo vimeharibika kabisa na jumla ya waliofoariki ni 42 na majeruhi ni 91.
Rufunga amesema mpaka sasa majeruhiwa wanaendelea vizuri na hali kwa sasa juu ya matibabu na dawa serikali imeweza kulisimamia ingawa kwa michango inaendelea ili kuweza kuwakimu walioathirika na maafa hayo.
Aidha amesema kwa sasa kambi ni moja ambayo wameiweka katika shule ya msingi makwaka lakini jitihada za kutafuta maehma ili kuwahamishia waathrika katika maeneo ya muinuko inaendelea.
No comments