Breaking News

NEWS Zitto Aendeleza Moto Bungeni, Aibua Ufisadi Mwingine Wa Trilioni 6.8

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akiwa kazini Bungni, Mjini Dodoma
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akiwa kazini Bungeni, Mjini Dodoma

Wakati Bunge la 11 likiendelea kurindima Mjiji Dodoma, tayari kashfa mbalimbali zimeanza kuibuliwa huku wabunge wakihitaji maelezo ya kina ikiwa ni pamoja na kuitaka Serikali kuchukua hatua stahiki.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amefikisha bungeni sakata la ufisadi wa zaidi ya Shilingi Trilioni 6.8 uliotokana na mkopo wa Serikali kupitia Benki ya Stanbic yenye tawi lake nchini, huku akiitaka Serikali kuelezea hatua iliyochukua dhidi ya watumishi waliohusika na sakata hilo kwa kupokea hongo ili kuongeza kiwango cha riba ya mkopo huo.
Zitto aliyasema hayo alipokuwa akiuliza swali la nyongeza na kuhoji “Je Serikali haioni kwamba umefika wakati Mkaguzo na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum wa mikopo yote ya kibiashara ambayo Serikali imechukua katika kipindi hicho husika ili kuweza kujua kama kulikuwa na aina za rushwa za namna hiyo ambazo zimekuwa zinafanyika?”
Zitto pia alitaka kufahamu kama Serikali ina nia ya kuifungulia kesi Benki hiyo ya nchini Uingereza baada ya kutoa hongo kwa watumishi wa Tanzania waweze kufanikisha ufisadi huo.
Akijibu maswali ya Mhe. Zitto, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amesema kuwa CAG ana wajibu kikatiba kufanya uchunguzi huo ili kujiridhisha kuhusu utaratibu uliotumika kutoa mikopo kupitia makampuni hayo na kama kuna dalili zozote za wizi, rushwa na ufisadi.
Masaju alimtaka Zitto kushirikiana na vyombo husika ikiwa ni pamoja na ofisi yake na kuwasilisha ushahidi utakaosaidia hatua stahiki kuweza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kufungua shauri mahakamani

No comments