Breaking News

27 Feb 2015 ALBINO KWENDA UMOJA WA MATAIFA KUISHITAKI SERIKALI

Watu wenye ulemavu nchini wamesema hatua zisizoridhisha zinazochukuliwa na serikali dhidi ya vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na wengine kusababishiwa ulemavu wa kudumu zinawasukuma kuishtaki serikali kwenye umoja wa mataifa ambako serikali imeridhia na kusaini mikataba yote ya kimataifa ya kumlinda mtu mwenye ulemavu.

Tamko hilo la watu wenye ulemavu linatolewa jijini Arusha na wadau waliokutanishwa na program ya jumuiya ya makanisa duniani inayoshughulikia utetezi wa watu wenye ulemavu kujadili ujumuishaji wa watu wenye ulemavu katika nyanja za maendeleo.
 
Akizungumzia mauaji hayo katibu wa shirikisho la watu wenye ulemavu nchini Bwana Felician Mkude anasema ni jambo la kushangaza kuona kuwa serikali imekua ikielekeza nguvu kubwa pale wanyamapori wanapouawa tofauti na mauaji ya watu wenye Albinism yanapotokea, lakini akaenda mbali zaidi na kuzungumzia nguvu kubwa iliyoelekezwa kuwashughulikia majambazi waliojitokeza jijini Tanga hivi karibuni akihoji ni kwa nini nguvu hiyo hailekezwi kwa kundi hilo lililokosa amani.
 
Kwa upande wao wanaharakati wa haki za watu wenye ulemavu kutoka asasi ya sasa foundation Bi Jovita Mlay na Bi Mackrine Rumanyika wakazungumzia umuhimu wa jamii yote kushiriki kuwalinda watu wenye ulemavu kwa kuanzia ngazi ya familia.

No comments