Breaking News

27 Feb 2015 WALIOMTEKA MTOTO ALBINO PENDO EMANUEL WAMESHAKAMATWA 14 HADI SASA

Jeshi la polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu 14 kwa tuhuma za kuhusika na tukio la utekaji nyara wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Pendo Emanuel wa kijiji cha ndami wilayani kwimba lililotokea Desemba 27 mwaka jana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa mulongo akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya za Misungwi, Kwimba na Sengerema amesema kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao wamo waliohusika kwenye utekaji wa mtoto huyo pamoja na wale waliomuhifadhi kwenye hoteli moja jijini Mwanza kabla ya kumsafirisha kwenda kusikojulikana. 
 
Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la kuwaapisha wakuu hao wapya wa wilaya hizo tatu za mkoa wa Mwanza, ambao ni Pily Moshi wa Kwimba, Zainabu Telack wa Sengerema pamoja na Mwajuma Nyiluka wa Misungwi, mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo akabainisha zilizofikiwa katika kuwasaka watu wanaotuhumiwa kumteka nyara mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Pendo Emanuel na kutokomea kusikojulikana.
 
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Mwanza Alfred Kapole pamoja na katibu wa chama hicho mkoani humo Enos Tuju wameendelea kupaza sauti zao kwa kuiomba serikali kudhibiti vitendo vya mauaji ya albino yanayotokea Mwanza.
 
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza Acp Japhet Lusingunaye akawa na neno juu ya hatua zilizochukuliwa na jeshi la polisi kuhusiana na mauaji ya watu takribani 16 wenye ulemavu wa ngozi yaliyotokea katika mkoa wa Mwanza peke yake

No comments