Home
/
Www.dj abasi.blog.com
/
27 Feb 2015 Chid Benz Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwili Jela au Kulipa Faini ya sh. 900,000
27 Feb 2015 Chid Benz Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwili Jela au Kulipa Faini ya sh. 900,000
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa hayo.
Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.
Hata hivyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana imemwachia huru mwanamuziki huyo baada ya kulipa faini ya 900,000/
27 Feb 2015 Chid Benz Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwili Jela au Kulipa Faini ya sh. 900,000
Reviewed by Unknown
on
February 27, 2015
Rating: 5
No comments