Breaking News

27 Feb 2015 MAJANGILI SASA KUNG'OLEWA MENO WAKIKAMATWA, KAMA WANAVYOWAFANYIA WANYAMA

todayViongozi wa dini wameshauri majangali watakaokamatwa na kuthibitika kufanya ujangili, wang’olewe meno ili wasikie uchungu wa kufanya vitendo hivyo kwa wanyama.

Aidha alionya ni wakati kwa waovu hao kufika mwisho na kuacha ujangili wa kuua wanyama na kuchezea rasilimali nyingine za nchi bila kuchukua hatua.

Baddhi ya viongozi hao wadini walionya kulegalega kwa viongozi wa Serikali na kushindwa kukabiliana na ujangili na kwamba hali hiyo ni kuwadanganya wananchi katika jambo kubwa linalohusu uchumi wao.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Musa Salum alisema umefika wakati wa viongozi wa dini kujitokeza waziwazi na kuisaidia Serikali katika vita dhidi ya ujangili.


Askofu Joseph Mwingira alisema  Serikali ina dhamana ya kulinda rasilimali  kama itasimamiwa vizuri ujangili utaisha na umaskini nao utaisha

No comments