Breaking News

27 Feb 2015 Mh. Al Shaimar Kweigyir amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino)

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiTlpcKueuYSxRLtCOMZnyJDZiz-5ttonOsT9s3eoMy18yXvoQNLeVr9xOcQdFZlW-2XubU7WRTFktLwmhGQQiECfLYQXmQLfsgej2xib2dUHal9Oz1ThyphenhyphenRJ49eGTGiaY_wlWXHsGLflPE/s1600/Mgonjwa.jpg 
Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Mbunge wa kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir,
amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi
albino,Yohana Bahati, aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa.


Katika ziaraa hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini
Mwanza, Mh Shaimar aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa
wa Mwanza, Crencencia Joseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Bayport
Financial Services mkoani Mwanza. 


Wakiwa Hospitali ya Bugando, Mbunge Shaimar na alioambatana
nao alipata fursa ya kuzungumza na wahudumu katika wodi aliyolazwa Ersther
ambaye ni wa Yohana na kumfariji katika kipindi kigumu cha kuuguza majeraha
yake pamoja na kulia msiba wa mwanae.


Tukio la utekaji na uporwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi
limezidi kushika kasi, ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau,
hususan wale wenye ulemavu wa ngozi wakiamini kuwa serikali imeshindwa
kuwapatia ulinzi wa kutosha.


Akiwa jijini Mwanza, Mbunge Shaimar na taasisi ya kifedha ya
Bayport Financial Services watakuwa kwenye safari ya kuelekea wilayani Kwimba
kwa ajili ya kwenda eneo alilokuwa akiishi Ester na watoto wake, hususan wawili
kati ya watano waliobaki wakiwa ni albino

No comments