Breaking News

27 Feb 2015 Rais Lungu wa Zambia aandaa Dhifa Kwa Heshima ya Rais Kikwete


1
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais wa Zambia Edgar Lungu pamoja na wake zao Mama Salma Kikwete na Mama Esther Lungu wakinyanyua glasi juu wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake ambao walifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Zambia.
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Edgar Lungu wa Zambia wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.
3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na Rais wa Kwanza wa taifa la Zambia Dkt.Kenneth Kaunda wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili nchini Zambia tayari amerejea jijini Dar es Salaam. (picha na Freddy Maro)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Zambia kwa ajili ya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais Edgar Lungu ( mwenye suti ya kijivu aliyesimama mbele ya Rais Kikwete).
Rais Lungu akimkaribisha Rais Kikwete (hayupo pichani kuzungumza).
Mhe. Rais Kikwete akizungumza wakati wa mazungumzo rasmi na Rais Lungu na Ujumbe wake katika Ikulu ya Zambia. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe na kulia ni Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salum na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma

No comments