Breaking News

Marehemu John Komba Asimangwa Mitandaoni, Familia Yalalamika

MTOTO wa aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), John Komba, amelalamikia baadhi ya wananchi wanaosambaza kashfa za baba yake. Anaripoti Sarafina Lindwino…

Gerald Komba, mtoto wa tatu wa hayati John Damian Komba amesema, mitandao mingi ya kijamii kumejaa “nukuu chafu za baba yake.” Nukuu hizo, ni zile mbazo alizitoa wakati wa uhai wake.

“Ninawaomba Watanzania wenzagu kuacha kusambaza maneno ya kashfa kwenye mitandao, haswa baada ya mhusika kufariki dunia,”ameeleza Gerald.
 
Gerald ameeleza jinsi anavyoumizwa na maneno ya mitandaoni kuhusiana na kifo cha baba yake.
 
Ametaja moja ya nukuu ambayo imeshika kasi kwenye mitandao ya kijamii, ni ile ambayo baba yake aliitoa katika kipindi ambacho mjadala wa Katiba Mpya ulipamba moto.
 
Mwanasiasa huyo alijiapiza kuwa ikiwa “Katiba mpya yenye muundo wa Serikali Tatu itapita, nitaingia mstuni.”

“Sasa imetosha. Nawaomba wamuache baba yangu. Kama alihukumiwa tangu akiwa hai, basi huu sasa uwe muda wa kumuombea ili aweze kupumzika kwa salama,” ameeleza kwa sauti ya unyonge.
 
Amesema, “Nawaomba wananchi wenzangu, waachane na maneno hayo. Yanaumiza familia. Tumuache Mungu atoe hukumu yake juu yake.”
 
Maneno mengine ambayo yanakumbukwa kwa Komba ni pale aliposema, “Warioba shida. Shida. Shidaaaa.”


Nukuu nyingine ambayo Komba ametwishwa katika mitandao ya kijamii ni ile inayosikika akisema, “…Chadema haitochukua madaraka wakati bado nikiwa hai

No comments